Usiku Mtakatifu (KISWAHILI)
From Mwimbieni Bwana (1988 - Evangelical Lutheran Church of Tanzania)

Usiku mtakatifu!
Wengine walala
wakeshao ni Yosefu tu
na Maria waliomlinda
Yesu mwana mzuri
Yesu mwana mzuri.

Usiku mtakatifu!
Wachunga wapewa
habari nzuri na malaika,
zienezwe popote sasa:
Yesu mponya kaja
Yesu mponya kaja.

Usiku mtakatifu!
Siku ya furaha
imetuangaza Kimungu
tumeupewa ukombozi
Kristo amefika
Kristo amefika.


Kengele za Juu (KISWAHILI)
 
Zanena, Sikukuu
Kengele, za Juu
Waumini furahini
Mukombozi mkumbusheni
Mzawa leo Betlehem
Mzawa leo Betlehem.


 

Submitted by: Keiron White, Edith Lyimo & Lars Bernhard


Return to Homepage
Return to homepage